Mkazi
wa Mandewa, Manispaa ya Singida, Said Mamba (24), amelazwa katika
hospitali ya mkoa mjini Singida baada ya kung’atwa theluthi tatu ya
ulimi wake na mwanamke waliyekuwa wakinyonyana ndimi.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Septemba 12, saa 3:30 usiku wa sikukuu ya Idd el Hajj.
Mamba, ambaye hawezi kuzungumza ametoa maelezo ya tukio hilo kwa njia ya maandishi.
Alisema
siku ya tukio alikutana na mwanamke huyo kwenye grosari iliyopo eneo la
Mandewa na baadaye mwanamama huyo alimwomba amsindikize nyumbani
kwake.
“Nilikubali
kumsindikiza, tukiwa njiani aliniomba tufanye mapenzi. Nilipokataa
alinilazimisha na baada ya kuona sitaki aliomba tuagane kwa kunyonyana
ndimi, nilikubali ombi hilo,” alisema.
Mamba
alisema wakati wakiendelea, mwanamke huyo alianza kumvua mkanda wa
suruali lakini alimzuia ndipo alipomng’ata ulimi na kuondoka na
kipande.
Mzazi
wa Mamba, Fatuma Alli alisema alipata taarifa ya tukio hilo baada ya
siku tatu na kwamba, siku hiyo hiyo mume wa mwanamke aliyetenda kitendo
hicho alikwenda kwake akieleza kijana huyo alijaribu kumbaka mkewe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Peter Kakamba, alisema hana taarifa za tukio hilo.
Daktari
wa meno wa hospitali hiyo, Dk Hamisi Kakandilo alisema ulimi wa kijana
huyo hauwezi kutibika isipokuwa kuusafisha ili asipate maambukizi.
“Hata kama kipande kilichotolewa kingepatikana kisingeweza kushonwa,” alisema.
Friday, September 16, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment