Kanichambua kama karanga mama. Chambua kama karangaaa
Good morning mabibi na mabwana. Inatia moyo sana kuona msanii kutoka
bongo land anaweka rekodi na kuivunja mwenyewe. Mpaka sasa hakuna msanii
yeyote barani afrika ambaye Video zake zinatizamwa na watu wengi ndani
ya muda mfupi kama Mondi Platnumz.
Sio kuwa tunajivunia Viewers ila tunajivunia Mziki wetu kutoboa zaidi Anga za kimataifa.
Japo kuna watu wachache walioanza kuleta chokochoko na kutaka wimbo huu
mpya ufungiwe kwa madai ya kutokuwa na maadili ila wengi wetu
tunampongeza kwa ubunifu na kumsaidia Bi Saida karoli kurudi tena
masikioni mwa watu. Binafsi baada ya kusikia wimbo huu niliamua
Kudownload na wimbo wa Saida karoli ili nione kama ameutendea haki wimbo
huo.
Hongera Diamond platnumz na tunatarajia leo Tutahit 1M viewers ikiwa ni siku ya pili baada ya Salome Kufufuliwa.
Ujumbe wa leo " WENYE WIVU WAJINYONGE"
0 comments:
Post a Comment