-Kulikuwa na kishindo mjini Mombasa wakati waandalizi wa sherehe za kusherehekea miaka 10 tangu kubuniwa kwa ODM walipomfanya msanii Diamond Platinumz kutumbuiza kabla ya mshindani wake mkuu, Ali Kiba
Kulikuwa na kishindo wakati wa tamasha ya kusherehekea miaka 10 tangu kubuniwa kwa chama cha ODM- Mama Ngina, Jumamosi, Septemba 10, 2016.
Diamond alikuwa anaondoka jukwaani kwa madaha baada ya kutumbuiza umati wa watu alipogundua alikuwa amemtangulia mshindani wake mkubwa nchini Tanzania, Ali Kiba.
Mtangazaji wa KTN Jamal Gadaffi ndiye aliyekuwa mfawidhi wa sherehe hiyo alimuita Ali Kiba kutumbuiza baada ya Diamond.
Wengi walitazamia kuona Ali Kiba akitumbuiza kabla ya Diamond ambaye anasemekana kuwa msanii bora.
Kuzidi kukaa kwake jukwaani hata baada ya kutumbuiza kulizua rabsha huku umati ukitaka kujua kilichokuwa kinaendelea.
0 comments:
Post a Comment