Friday, September 16, 2016

HUKUMU ya Kumlawiti Mwanaye yamfanya Ajiue Kwa Kunywa Sumu

Hassan Mtiko (49) amejiua kwa kunywa sumu, muda mfupi baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 60 jela kutokana na kupatikana na hatia ya kumbaka na kumlawiti  mwanaye mwenye umri wa miaka 11.

Tukio hilo  lililotokea  juzi mchana eneo la Bomang’ombe mjini Hai, limezua gumzo maeneo mbalimbali ya mji huo.

Mfungwa huyoalikunywa sumu akiwa mahabusu ya Kituo cha Polisi Bomang’ombe wilayani Hai, muda mfupi baada ya kuwaomba ruhusa askari kwenda chooni kujisaidia.

Chanzo cha habari kilieleza kuwa baada ya kuhukumiwa adhabu hiyo, mfungwa huyo alipelekwa mahabusu ya polisi akisubiri kupelekwa gerezani.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, mahabusu  walianza kumuona akiugulia maumivu  na kutoa taarifa kwa askari mahakamani hapo.

Baada ya kunywa sumu hiyo juzi mchana, mfungwa huyo alipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Hai  na kufariki dunia jana mchana.

0 comments:

Post a Comment