Serikali
imetenga kiasi cha shilingi bilioni 5.09 kwa ajili ya kutoa posho ya
motisha ya madaraka kwa walimu wakuu, wakuu wa shule na waratibu elimu
kata ili kuwa na usimamizi mzuri wa sera ya elimu bure ili iweze kuleta
tija kwa taifa.
Hayo
yamezungumzwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa kwenye
hotuba yake ya kuahirisha bunge iliyokuwa inazungumzia mambo mbalimbali
ya kiserikali na shughuli za bunge.
Waziri
Majaliwa amesema kuwa serikali imeanza kutoa pikipiki kwa waratibu
elimu kata kila mkoa nchini ili ziwawezeshe katika ufatiliaji na
usimamizi wa shughuli za kielimu katika kata zao nchi nzima.
Waziri
Majaliwa amesema kuwa kwa kuanzia tayari waratibu kata wa mikoa 7
ambayo ilikuwa na ufaulu wa chini katika matoke ya kuhitimu darasa la
saba na tayari wameshapatiwa jumla ya pikipiki 1015.
Aliitaja
mikoa hiyo iliyopata pikipiki hizo ni pamoja na Mkoa wa Dodoma,
pikipiki 192,mkoa wa Mara 99, Simiyu 122, Shinyanga 128, Tabora 200,
Kigoma 135 na Lindi Pikipiki 139.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu amesema kuwa katika kukabiliana na upungufu
wa walimu serikali imeamua walimu watakaoajiriwa mwaka 2016 wapangwe
shuleni moja kwa moja na kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa wa walimu.
nice kka
ReplyDelete