Msanii wa muziki wa Hip Hop anayefanya vizuri na wimbo ‘Chafu Pozi’
Billnas amesema yupo kwenye mazungumzo ya kuhamia katika label kubwa ya
muziki hapa nchini hivi karibuni.
Rapper huyo ambaye kwa sasa yupo chini ya label yake ya ‘LFLG’,
ameiambia Bongo5 kuwa kuna label nyingi zinamtaka kufanya naye kazi.
“Kusema kweli kuna mambo makubwa yanakuja, huwenda kazi yangu mpya ikaja
nikiwa ndani ya label mpya,” alisema Billnas. Kuna label nyingi
zimekuja na bado nipo kwenye mazungumzo, nadhani muda ukifika mtasikia
tu,”
Billnas alianza kufanya vizuri na wimbo ‘Ligi Ndogo’ akiwa Rada
Entertainment lakini baadae alihama katika label hiyo na kuanzisha label
ya ‘LFLG
Friday, September 16, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment