Wanaume wengi hupuuzia hili, huona kama ni jambo lisilo na maana sana
kwao na wenzi wao. Hali ni tofauti sana kwa wanawake ambao hupenda
kuwasifia wanaume zao. Nitakupa mifano miwili ya namna wanandoa wa
jinsia mbili tofauti wanavyotambulishana kwa jamaa zao. Kwa mafano
manakutanata kwenye majumuiko ya harusi na sherehe kama hizo. Mme 1
akamtambulisha mkewe kwa jamaa zake, huyu ni mama Rick mke wangu. Mme wa
2 akamtambulisha mkewe, huyu ni my lovery sweetheart wife, nampenda
sana kuliko wanawake wote duniani. Kama upo kwenye huu utambulisho
umeona tofauti gani? hao wanawake wa pande mbili watajisikiaje? Nahisi
umejifunza kitu hapo
MALENGO SHIRIKISHI
Wanaume wengi wana ulemavu mmoja; hawapendi kuwashirikisha wanawake
katika mambo yao. Wanapenda kufanya mambo yao kwa siri na wakati
mwingine ikilazimika kumwambia mkewe basi kwa mshtukizo baada ya
kukamilisha jambo husika. Siku hizi dunia imebadilika, kuna mambo mengi.
Kuna suala la hasara katika biashara, utapeli, kifo cha gafla, ajali
n.k. Mkeo ndiye rafiki yako mkubwa kuliko wote, ndiye ndugu yako wa
karibu zaidi kuliko yeyote. Mmeshirikiana kuzaa watoto na kujenga maisha
pamoja. Yeye anapaswa kujua mambo yako, ndiye mtetezi wako nambari
wani. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia
sehemu ambayo hukutarajia. Hata hivyo, kumshirikisha katika malengo
yako, kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu.
Lakini ngoja nitoe angalizo, kuna wanawake ambao huwezi kumshirikisha
from A to Z ya malengo yako kutokaa na tabia na mienendo ya maisha, hope
kila mtu anafahamu strength and weakness ya wake na waume zetu, so be
careful in some extent.
KIPAUMBELE/CONCERN
Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia.
Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama
nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mkeo akawa katika hali hiyo,
msikilize. Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi
wake anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako
tu, kutampa matumaini na faraja kwamba anaishi na mtu sahihi. Acha
kupuuza mambo yake; hata yale madogo, kama ya ‘mtoto wa dada amerudishwa
ada shuleni’. Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza
msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una
tatizo binafsi, kikazi au kifamilia, mshirikishe. Unaweza kushangaa
jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha
likawa jepesi zaidi na mambo yakaenda vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote
ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa mwanamke.
"Together we swim in the same pool"
USAFI
Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda sana usafi. Ni aghalabu kukutana na
mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au ua la
nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi. Mwanamke
anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini
kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata
anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebeleni hadi
chumbani. Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye
kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele. Rafiki yangu, kama uko
mbali na usafi, ujue kuwa itakuwa vigumu kupata mdada wa ukweli – yule
wa ndoto zako. Wanaume wengine wanapanga kutoka outing na wapenzi wao,
mkifika huko mwanamke anajuta WHY amekubali kukutana na wewe maana
utamkuta mwanaume hajapasi Tshirt/shirt, kwapa linapumua, ukiongea mdomo
unatoa harufu inakuwa tabu tupu. Mwanume ukijipenda unatakuwa
mtanashati tu
KUJIAMINI
Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini –
mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia. Siyo anayebabaika.
Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia
manukato mapya! Mathalani unakuwa naye katika mtoko, angependa kukuona
ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa
maamuzi yasiyoyumba. Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata
katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako,
lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.
Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwenye kujiamini na mawazo yasiyo
na matege wala makengeza! Usiyebadilika kama kinyonga! "Men believe on
your standing hills"
ANAYEJALI na KUFUATILIA
Wanawake wanapenda sana wanaume wanaowajali. Wanaowaona wao ni kila kitu
na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika
nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi wako kwa kila hali
lakini pia uwe na kiasi. Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua
maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa ya kuendelea kudumu katika
uhusiano hai. Wanaume wengi ni wavivu, si tu kuwatumia hata SMS za
“mambo dia?” wapenzi wao lakini hata kujibu tu, “niko poa, Si hulka ya
wanaume kutumatuma SMS – inajulikana, lakini angalau ukiweza kulifanya
hili hata kidogo tu hata mara moja kwa wiki, utakuwa unajiongezea pointi
kwa mwenzi wako na kumpa courage ya kufurahia mapenzi ya ndoa.
MAANDALIZI YA TENDO LA NDOA
Tendo la ndoa halina maana ya kukomoana. Jenga mazoea ya kufanya
maandalizi kamili kabla ya tendo. Sikiliza hisia za mwenzako. Ukiweza
kumjulia mke wako katika eneo hili, ni wazi kwamba utazidisha upendo
wake kwako, lakini pia atakuwa katika kuta za uaminifu. Unapokuwa kazini
mchokoze "aisee nasikia hamu leo" hayo ndo maandalizi ya saikolojia.
kupitia sms hiyo utasikia feeling zake, ataji-express. Kufikia
jioni/usiku utashangaa unashikwa mkoni kupelekwa kitandani. Akatafute
nini nje wakati wewe ndiye mganga wake unayeweza kumtibu barabara?
Jiamini katika shughuli, fanya mazoezi ya viungo hata kukimbia ili
uongeze pumzi ya kutoa dozi kitandani.
Epuka mapenzi ya kubakana, unafika tu bed unamvuta unamvua na kuanza
kupanda kifuani......nooooooo hapo hakuna maandalizi ya kisaikolojia
wala ya kimwili, hii itampekea kuchukia tendo because there is no any
enjoyment
OUTING SOMETIMES
Kulingana na budget yako, si vibaya mara moja kumtoa mpenzi wako outing
walau mara moja ndani ya miezi sita hata mwaka kama budget ni shida. Kwa
wale wenye familia unaweza toka mkaspend 1 or 2 days outing na mkeo.
Kuna mambo mmeo/mkeo anaogopa kukufanyia kulingana na mazingira ya hapo
nyumbani na familia kwa ujumla. Lakini mkitoka nje LAZIMA mta-experience
the difference for SURE. Pia ni njia mojawapo ya kuboresha na kupalilia
penzi lenu na kuongeza uaminifu kati yenu
Naomba niishie hapo kwa leo
Friday, September 16, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment