Umati wa watu umepiga kambi eneo la Rujewa, wakisubiri tukio la kupatwa kwa jua kipete linalotokea baadaye leo.
Katika eneo hili ambalo awali halikuonekana kuwavutia wapita njia hata
kufaa kutumika kama sehemu ya kujiburudisha kutokana na shughuli ya
uchimbaji mawe na upasuaji kokoto, usiku huu watu wamejaa huku watu
wakijiburudisha.
Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia watu wakiingia na kutoka eneo hilo,
ambalo wataalam wa anga wameweka mitambo yao kwa ajili ya kuratibu
tukio hilo la kihistoria.
Mama lishe, wachoma nyama na wauzaji wa vinywaji vikali wapo kazini kuwahudumia watu waliofika kushuhudia tukio hilo.
“Kwa kweli tukio hili ni kukumbukwa, muda kama huu ninakuwa nyumbani
lakini hawa watu lazima wahudumiwe,” mamalishe Christina Mgaya.
Hata hivyo, uhaba wa nyumba za kulala wageni katika mji mdogo wa Rujewa
umesababisha baadhi ya wageni kukosa sehemu ya kulala na kukesha eneo
hilo.
Thursday, September 1, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment