Huenda Diamond Platnumz akawa ameitimiza ndoto aliyokuwa nayo kwa miaka mingi – kumiliki gari alipendalo zaidi, Rolls Royce.
Kwa muda mrefu, staa huyo amekuwa akisema kuwa hilo ndilo gari analotaka
kulimiki kiasi cha kujipa jina ‘The Rolls Royce Musician From East
Africa.’
Diamond ambaye yupo jijini Los Angeles, Marekani alikoenda kushoot video
ya wimbo aliomshirikisha Ne-Yo, ameshare kipande cha video kwenye
Instagram cha gari hilo na kuashiria kuwa huenda akawa amelinunua
tayari.
Hata hivyo hajasema iwapo gari hilo limeshakuwa mali yake ama alikuwa tu showroom kuosha macho!
Rolls Royce, ni magari yanayozalishwa na kampuni ya Uingereza na
yalianzishwa na Charles Stewart Rolls na Sir Frederick Henry Royce,
March 1906. Bei yake huanzia $300,000 – $500,000.
“Nataka nibadilishe aina ya gari sababu imekuwa ni muda mrefu, nafikiri
ni muda wa kuwa na gari nililokuwa nalitamani siku zote, gari la ndoto
yangu ni Rolls royce na ndio ninalotaka kulinunua mwaka huu wa 2016 na
litakuwa na jina la PLATNUMZ na sio namba za kawaida,” aliiambia tovuti
ya Millard Ayo miezi kadhaa iliyopita.
Alidai kuwa kwa alipofikia ni muhimu kwa na gari la hadhi yake ili kujiongezea thamani zaidi.
“Ndio maana nikipata Rolls Royce inatengeneza heshima,” alisema.
Thursday, September 1, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment