Katika kipindi cha mzunguko (siku za hedhi) kwa kawaida wanawake
hupoteza kiasi cha damu pamoja na baadhi ya madini chuma mwilini.
Hali hiuo huweza kusababisha upungufu wa damu kama mwanamke atakuwa
hapati lishe bora na ya kutosha. Sasa ili kuzuia upungufu wa damu na
madini mwilini, msichana anatakiwa kula vyakula vyenye madini chuma na
chokaa kwa wingi ikiwa ni pamoja na hivi vifuatavyo:-
Orodha ya vyakula vinavyopendekezwa
Mboga za majani
Maharage
Soya
Samaki
Maziwa
Korosho
Mayai
Dagaa n.k.
Mbali na vyakula hivyo, pia mwanamke huhitaji kuzingatia hali ya usafi
wa mwili, hasa sehemu za siri . Tumia vitambaa safi vilivyo nyooshwa kwa
pasi au pedi zilizohifadhiwa katika hali ya usafi.
Tuesday, September 20, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment