Sunday, September 20, 2015

Mh:EDWARD LOWASA KUITIKISA TENA LEO DAR ES SALAAM

MGOMBEA urais wa Chadema na anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa anatarajia kuliteka tena Jiji la Dar es Salaam leo  katika mikutano mitatu.

Lowassa anarejea tena jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya mikutano kwenye majimbo ya Kawe na Kibamba Septemba 7 mwaka huu na kunadi wagombea wa majimbo hayo.

Lowassa alimnadi John Mnyika wa Kibamba na Halima Mdee wa Kawe kabla ya kuelekea visiwani Zanzibar katika uzinduzi wa Kampeni za Urais za Maalim Seif wa CUF.

Jijini Dar es Salaam leo Lowassa anatarajia kufanya mikutano yake katika Jimbo la Ukonga, Kigamboni na jimbo jipya la Mbagala ambapo maandalizi tayari yamekamilika.

Lowassa ataanzia Jimbo la Kigamboni saa 3:00 asubuhi, saa 6:00 mchana atakuwa katika Jimbo la Mbagala na atamalizia kwenye Jimbo la Ukonga saa 9:00 alasiri.

Sambamba na viongozi wengine Lowassa ataambatana na timu nzima ya kampeni ya UKAWA akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye; aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja; meneja wa kampeni John Mrema pamoja na mwenyekiti wa Chadema-Taifa, Freeman Mbowe.

Lowassa anaingia Dar es Salaam akiwa tayari amezunguka kwenye mikoa 15 ya Tanzania ikiwemo Dodoma, Geita, Kagera, Geita, Shinyanga na Iringa huku mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Arusha na mingeneyo ikiwa bado kufikiwa.



0 comments:

Post a Comment