Diamond amedai kuwa Saida Karoli atapata asilimia 25 ya mapato ya wimbo wa Salome.
Diamond amerudia baadhi ya vitu kwenye wimbo wake mpya ‘Salome’
aliomshirikisha Raymond kutoka kwenye wimbo wa ‘Maria Salome’ wa Saida
Karoli uliotoka takribani miaka 16 iliyopita.
Akiongea na 255 ya Clouds FM Jumatatu hii, hitmaker huyo wa Kidogo
amesema kuwa walizungumza na uongozi wa Saida Karoli na kumpatia kiasi
cha fedha pamoja na asilimia 25 ya publishing ya wimbo huo.
“Kitu tulichokifanya kabla ya kurelease wimbo, tulizungumza na uongozi
wake, tukawaambia tunafanya hiki na hiki na kuna kiasi pia tukakitoa ili
kiende kwake halafu tukampa 25% ya publishing. Kila income ya
publishing ikiwa inaingia katika huu wimbo, mama atakuwa anapata
percent,” amesema Diamond.
Mpaka sasa video ya ‘Salome’ ya Diamond ina siku mbili tangu ilipoachiwa
kwenye mtandao wa YouTube lakini imefanikiwa kutazamwa mara 734,954 views.
Tuesday, September 20, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment