Mkuu
Anasema waathirika wasikae tu huko wanangoja hela za serikali kwa sbb
wanasikia zimechangwa,waanze kujisaidia kwanza wao na serikali
itawasaidia pale waliposhindwa.
Mkuu
anasema mtu ukuta umedondoka, anataka asubiri serikali ndio
imtengenezee! Watu wajue tetemeko ni janga la asili halijaletwa na CCM.
Waanze kwa kujenga wenyewe kuta zilizodondoka sio wasubiri serikali,
sababu maisha yanendelea na watu wanatakiwa wafanye kazi kwa kujenga
nyumba zao na sio kila kitu serikali itafanya.
Na
wale wanasiasa wanaotaka kutumia janga hili kujinufaisha kisiasa mkuu
anasema waache mara moja....Na kasema wote wanaotumia janga hili
kukusanya misaada kwa njia ya kitapeli, basi wakamatwe mara moja.
Saturday, September 17, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment