Serikali
imeshusha vigezo vya udahili kwa ajili ya kujiunga na vyuo vikuu katika
mwaka wa masomo 2016/17 kwa waombaji wanaotumia sifa mbadala
(Equivalent Qualification) ambao ni wenye Stashahada pamoja na FTC.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU),
kigezo cha ufaulu kwa waombaji wenye sifa ya stashahada (Diploma)
kimeshushwa kutoka GPA ya 3.5 hadi GPA ya 3.0, ili kutoa nafasi kwa
waombaji wengi zaidi kupata nafasi katika vyuo mbalimbali.
Taarifa hiyo pia imeshusha kigezo kwa waombaji wenye Full Technician Certificate (FTC) kutoka wastani wa B hadi wastani wa C.
TCU
imewatangazia wote wanaohitaji kuendelea na vyuo vikuu wenye GPA ya 3.0
kwa Stashahada na wastani wa C kwa wenye FTC watume maombi kupitia TCU
kabla ya Septemba 23, mwaka huu.
Pia TCU imesema kuwa wale ambao walikuwa tayari wamekwishatuma maombi, na wanakidhi vigezo hivi hawatakiwi kuomba tena.
Taarifa
hiyo ya TCU haijaweka wazi sababu za mabadiliko haya, ingawa tangu
kutangazwa kwa sifa mpya Julai 11 mwaka huu kumekuwa na malalamiko
kutoka kwa wadau mbalimbali wakitaka vigezo hivyo vilegezwe.
Friday, September 16, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment