Hivi
karibuni kumezuka tabia za utapeli unaofanywa na wanaojisadikisha kuwa
ni watumishi wa Umma au Mawakala wa kusimamia uhamisho wa Watumishi
kuhama kutoka Mkoa mmoja kwenda Mkoa mwingine na pia kujihusisha na
kutoa taarifa za uongo kwa kugushi nembo za Ofisi ya Rais.
– TAMISEMI kuhusu ajira, kupandisha madaraja ya walimu.
Yamekuwepo
Malalamiko mengi kutoka kwa wahanga/waathirika wa tabia hiyo kwa
nyakati tofauti ambayo watumishi wamehadaiwa kuwa watasaidiwa kuhamia
sehemu yoyote wanayoihitaji baada ya kulipa kiwango cha fedha ambacho
hupangwa na wahalifu hao. Miongoni mwa taarifa batili wanazosambaza ni
Uhamisho na Ajira za Walimu.
Matangazo
hayo pia yameonekana katika mbao za matangazo za baadhi ya Halmashauri.
Mara nyingi watu hao huweka namba zao za simu kwa ajili ya kupokea
fedha za uhamisho kutoka kwa watumishi pamoja na kuweka anuani za barua
pepe zinazosadikiwa kutumika katika kukusanya barua za maombi ya
uhamisho.
Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) inapenda
kuchukua fursa hii, kutoa taarifa hii kwa lengo la kuujulisha Umma wa
Watanzania juu ya kuwepo kwa uhalifu huu ili waweze kujiepusha nao.
Ofisi ya Ras –TAMISEMI haitasita kuchukua hatua za Kisheria kwa wale wote watakaobainika kujihusisha na uhalifu wa aina hii.
Tunasisitiza
kuwa wananchi wafuate taratibu na pia watambue kuwa hakuna malipo
yoyote yanayotakiwa ili kuhamisha mtumishi. Wananchi wanaombwa kutoa
taarifa pale watakapoona kuna utapeli unaoendelea katika masuala ya
ajira na uhamisho.
Watumishi
wanaweza kufahamishwa juu ya taratibu za uhamisho katika Ofisi za
Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri na pia kupitia
tovuti ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz).
Ofisi ya Rais TAMISEMI haijatoa matangazo yoyote yanayohusiana na Ajira za Ualimu katika kipindi hiki.
Imetolewa na:-
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
15 Septemba, 2016.
Friday, September 16, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment