Msanii
mkongwe na asiyesahaulika katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya dudu
baya amekivua nguo kituo cha clouds fm kwa kuwaita ni wanafki wakubwa,
wanyonyaji wa wasanii, na wenye kuharibia wasanii ndoto za mziki wao
Mamba
alitolea mfano wasanii wanazungushwa mikoani kwenye tamasha la fiesta
na kuambulia ujira mdogo, huku akisema pesa wanayopata kwenye hilo
tamasha huishia hukohuko mikoani na hurudi dar wakiwa wamepayuka hawana
kitu mfukoni
Dudu alisema hayo akipokuwa kwenye kipindi cha usiku cha FRIDAY NIGHT LIVE... FNL kinachorushwa na EATV
Alienda
mbali zaidi kwa kumpongeza msanii mwenye kipaji anayekuja juu ruby kwa
kusema ametoka kwenye minyororo ya wafu FM akawasihi na wasanii wengine
wamuige ruby kwani ameonesha mfano
Akionekana
mwenye afya km alivyokuwa zamani, amesema wafu fm hawajapiga nyimbo
zangu kwa miaka sita sasa lakini sijatetereka naendelea na maisha yangu
kama kawaida
Wakati
akiendelea kuwatolea uvivu clouds fm mtangazaji wa kipindi hicho sam
misago alitumia mbinu ya ziada kumtoa kwenye kile akichokuwa nacho
moyoni
Hata
hivyo alipongeza redio ambazo zipo chini ya IPP km East africa radio,
radio one, capital fm na kusema hajawahi kuombwa pesa na mtangazaji au
dj yeyote wa kituo hicho ili wimbo wake uchezwe hewan
Amevitaka vituo vingine kuiga vyombo vya ipp media
Kwa maneno ya dudu baya ni dhahiri wasanii wengi ni watumwa wa baadhi ya media house
Saturday, September 17, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment