Saturday, September 17, 2016

Nuh: Siwezi Kurudiana Na Shilole

MSANII wa Bongo Fleva anayetamba na Wimbo wa Jike Shupa, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amesema kuwa japo kuna tetesi zinaenea mtaani kwamba amerudiana na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ suala hilo halina ukweli wowote ndani yake na wala hafikirii kabisa kurudiana na mwanadada huyo.

Tetesi za Nuh kurudiana na Shilole zilianza kuvuma baada ya kusambaa kwa kipande cha video kilichowaonesha wakipatanishwa wakati wakiwa kwenye safari za Tamasha la Fiesta na watu kujiongeza kuwa wamerudiana.

Nuh Mziwanda akiwa na mpenzi wake wa zamani Zuwena Mohammed ‘Shilole’.

“Kilichotokea ni kwamba mimi na Shilole tumeondoa tofauti zetu za kibinadamu ambazo tulikuwa nazo baada ya kuachana.

Lakini kuhusu kurudiana hahitakuja kutokea hata siku moja na siwezi kurudi nyuma kwenye hili maana nina mpenzi wangu ninayempenda,” alisema Nuh.

0 comments:

Post a Comment