Kikosi
maalum cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha cha Jeshi la Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam kimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 5 wa
makosa ya ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali.
Kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Saimoni Sirro akionesha baadhi ya vifaa vilivyokamatwa.
Taarifa
hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam
Kamishna Saimoni Sirro wakati akitoa taarifa ya kukamatwa majambazi wa 5
na kukutwa na silaha aina ya shotgun, bastola 3 na risasi 49.
Katika
tukio lingine Polisi mnamo tarehe 5.9.2016 majira ya saa 8 usiku maeneo
ya Magomeni mtaa wa Makumbusho waliokota begi lililokuwa na bastola
mbili, sambamba na hilo wamefanikiwa kukamata magari 4 ya wizi, hati za
magari na watuhumiwa wawili wa uhalifu huo wamekamatwa.
Jeshi
hilo limetoa wito kwa viongozi wa serikali za mitaa kupitia kamati za
ulinzi wa mitaa kuimarisha ulinzi na kuwataka wamiliki wa nyumba za
kupanga kuhakikisha wanaweka kipengele cha kuwepo na picha katika
mikataba ya kupangisha nyumba zao kutokana na uwepo wa wimbi la uhalifu.
Wakati
huo huo Kamanda Sirro amesema Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kipindi
cha siku 11 wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 882,570,000 ikiwa
ni tozo za makosa ya usalama barabarani na makosa mengineyo.
0 comments:
Post a Comment