TERRY KUWAKOSA LIVERPOOL IJUMAA.
Nahodha wa Chelsea John Terry atakuwa nje kwa siku kumi bada ya kupata majeraga kwenye mguu wake wakati wa mchezo wa Ligi ya England mwishoni mwa wiki dhidi ya Swansea ambapo walitoka sare ya mabao 2-2, mchezo uliopigwa Uwanja wa Liberty.
Majibu ya vipimo alivyofanyiwa jana yanaonesha kuwa ataukosa mchezo wa Ijumaa dhidi ya Liverpool utakaopigwa Stamford Bridge.
Baada ya mchezo wa Jumapili meneja Antonio Conte: “Sifahamu kiasi gani amepata maumivu lakini kesho (Jumatatu) tutapata kujua kuhusu ankle yake. Lakini ni mpiganaji yule. Sina shaka naye worried.”
Kukosekana kwa John Terry ni ni nafasi kwa beki wa kimataifa wa Brazil David Luiz, ambaye amerejea Stamford Bridge akitokea Paris St-Germain kwenye dirisha la kiangazi lililofngwa hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment