Monday, January 5, 2015

MWIGIZAJI DOKII ATANGAZA KUSAKA MWANAUME WA KUMUOA 2015


MSANII wa filamu na muziki Ummy Wenslaus ‘Dokii’ amefunguka kuwa ndani ya mwaka 2014 hajapata mwanaume wa kuendana naye hivyo endapo akibahatika kupata mwenye upendo wa dhati mwaka huu, atampa kila kitu anachokihitaji.

Akipiga stori na paparazi wetu, Dokii alisema kitu kikubwa kilichomfanya awatoe wanaume moyoni kwa mwaka 2014 ni kutokana na wengi wao kutokuwa na upendo wa dhati.

“Siwezi kuwa na mpenzi wakati kila siku naona wenzangu wanalia, sijui nitapata wapi mwanaume mwenye upendo, wengi wapo kwa ajili ya kufanya ngono na mwisho wa siku wanakuumiza,” alisema Dokii.

0 comments:

Post a Comment