Wiki iliyopita Ikulu ya Nigeria kupitia kwa muandishi wa hotuba za Rais,
iliingia kwenye skendo ya kunakili hotuba ya Rais Barack Obama na kumpa
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ambaye aliisoma kama ilivyo bila
kujua, mpaka wapinzani walipoanzisha mzozo juu ya suala hilo.
Official responsible for Plagiarism of Obama's Speech to be sacked
Sehemu ya hotuba ya Rais Buhari iliyonakiliwa kutoka kwenye hotuba ya
Rais Barack Obama aliyoitoa mwaka 2008 inasema “Change Begins With Me”
Mabadiliko Huanza Na Mimi, ikifahamika kwa jina la Hotuba ya Ushindi.
Ikulu ya Nigeria imeomba radhi juu ya aibu iliyomkuta Rais wa nchi hiyo
na kuahidi kumchukulia hatua kali za kinidhamu muandishi aliyesababisha.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Trust limesema kuwa kiongozi huyo msaidizi
wa idara ya mawasiliano ya Rais, ataondolewa kazini kutokana na uzembe
alioufanya. Muda mfupi tangu kutokea tatizo hilo, Taasisi ya Rais
kupitia idara ya mawasiliano kwa Umma imeripoti kuwa itaweka software
itakayokuwa ikigundua kama hotuba zote za Rais zimenakiliwa kutoka
sehemu nyingine.
Msemaji wa Serikali ya Nigeria amesema >>>Tumepanga kuchukua
hatua ya kuweka kifaa kitakachokuwa na uwezo wa kukagua na kugundua kama
hotuba za Rais zimenakiliwa kutoka sehemu nyingine kabla ya kumkabidhi
Rais,”
Kitendo cha Hotuba ya Rais Buhari kunakiliwa kutoka kwenye Hotuba za
Rais Obama, kimewafanya vyama vya upinzani nchini humo kusema kuwa ipo
siku Rais huyo atasaini nakala za kujiuzulu bila kujua kutokana na
kutozikagua kabla ya kuzisoma.
Tuesday, September 20, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment