Tuesday, September 20, 2016

Mwanamuziki Vanessa Mdee Ataja Ndoto yake Katika Muziki wa Bongo Flava

Mwanamuziki wa kike anayesumbua ndani na nje ya Bongo, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amesema ana ndoto kubwa.

Ndoto yake siku moja, kuwa msanii kutoka Tanzania atakayeshinda tuzo za heshima, Grammy.Anaamini kuwa, mwanzo wa kukaribia kuiishi ndoto hiyo umewadia.

Vee Money ni mmoja wa wasanii wa Afrika, waliochaguliwa kurekodi wimbo na mshindi wa Grammy na nyota wa RnB nchini Marekani, Trey Songz.

Shukrani kwa kipindi cha Coke Studio Africa (International Week) msimu wa 4, kinachomdondosha staa huyo.

Akiwa pia anawania tuzo ya Loeries za Afrika Kusini kwa kazi yake ya video bora, Niroge.

“Katika harakati zangu za kutafuta ushindi wa Grammy katika career yangu ya muziki, inanipa nguvu kufanya kazi kwa ukaribu na Trey Songz, ambaye alishawahi kushinda tuzo hiyo.” amesema Vanessa.
Msimu mpya wa Coke Studio utaanza mwezi ujao.

0 comments:

Post a Comment