Tuesday, September 20, 2016

Wema: Nilitaka mil 75 kuwa Salome, WCB wakanipa mil 50 nikakataa

Mwanadada Wema akiongea na kipindi kimoja cha redio leo mchana alipoulizwa yapi maoni yake kuhusu wimbo mpya wa Salome alisema wimbo ni mzuri sana na alitakiwa kufanya video lkn ilibidi walipe mil 75 kama gharama za yeye kutokea kwenye video lkn WCB walitaka kutoa mil 50 ndipo aliposhauriana na uongozi wake na kuamua kukataa.

"Ni kweli ningetokea kwenye video hiyo lakini walitoa pesa madafu,kaka mtangazaji siwezi kuuza sura kwa mil 50,ebu fikiria nimetumia karibia bilioni kutengeneza jina langu,nina biashara za mamilioni,leo Nassib anataka kunipa mil 50,that is not fair kwa kweli"

Mdau yapi maoni yako kuhusu gharama za huyu mlimbwende?

Mtoto wa Bilionea wa China Amnunulia Mbwa Wake iPhone 7 nane!

Wang Sicong, mtoto wa bilionea wa China, Wang Jianlin (mwenye utajiri wa dola bilioni 30), amemnunuliaa simu mpya, iPhone 7, nane mbwa wake.

Mbwa huyo aitwaye, Coco ameonekana kwenye picha za akaunti yake ya mtandao wa Weibo akiwa na simu zake hizo. “I don’t understand all the show-off posts on (social media),” yanasomeka maneno kwenye picha hiyo. “What’s the point? Don’t make me do it?”

DIAMOND Kumjaza Mapesa Saida Karoli, Hiki Ndicho Atamlipa

Diamond amedai kuwa Saida Karoli atapata asilimia 25 ya mapato ya wimbo wa Salome.

Diamond amerudia baadhi ya vitu kwenye wimbo wake mpya ‘Salome’ aliomshirikisha Raymond kutoka kwenye wimbo wa ‘Maria Salome’ wa Saida Karoli uliotoka takribani miaka 16 iliyopita.

Akiongea na 255 ya Clouds FM Jumatatu hii, hitmaker huyo wa Kidogo amesema kuwa walizungumza na uongozi wa Saida Karoli na kumpatia kiasi cha fedha pamoja na asilimia 25 ya publishing ya wimbo huo.

“Kitu tulichokifanya kabla ya kurelease wimbo, tulizungumza na uongozi wake, tukawaambia tunafanya hiki na hiki na kuna kiasi pia tukakitoa ili kiende kwake halafu tukampa 25% ya publishing. Kila income ya publishing ikiwa inaingia katika huu wimbo, mama atakuwa anapata percent,” amesema Diamond.

Mpaka sasa video ya ‘Salome’ ya Diamond ina siku mbili tangu ilipoachiwa kwenye mtandao wa YouTube lakini imefanikiwa kutazamwa mara 734,954 views.

BASI la New Force Lapata Ajali na Kuua Watu 12

Watu 12 wamefariki dunia papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya New Force kupinduka katika eneo la Ilongwe kata ya Kifanya, Mkoani Njombe na kupelekea vifo hivyo pamoja na majeruhi.

Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Mkoa wa Njombe na Dar es Salaam lilipinduka majira ya saa moja na dakika 40 usiku wa kumakia leo wakati likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Njombe.

Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na shirika la habari la taifa kutoka mkoani Njombe zinasema kati ya watu hao 12 wanawake ni nane akiwemo mtoto mmoja wa kike pamoja na wanaume wanne akiwemo mtoto mmoja wa kiume.

Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo amesema kuwa chanzo cha ajili hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo ambapo amesema kabla ya ajali kutokea tayari basi hilo lilikuwa limeyumba karibu mara tatu na baadaye kupinduka kabisa.

Katika tukio lingine la ajali iliyotokea mkoani Kilimanjaro katika msafara wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki imesababisha majeruhi wawili akiwemo afisa wa polisi pamoja na mwandishi wa habari wa shirika la habari la taifa ambao wote wamelazwa kwa ajili ya matibabu.

Hivi Kwanini Wanawake wa Kilokole Wengi Wana Roho Mbaya?

Habarini wadau,

Hili nina ushahidi nalo, wengi wao nimegundua wana roho mbaya kwakweli na nina mifano mingi tu.

Yaani hao huwa wanaona kama watu wengine wasio walokole ni waovu tu. Niliwahi kushauriwa kuwa ni bora umuoe msichana aliyecharuka na kupitia starehe zote za dunia akatulia kuliko anayejiita mlokole namimi sasa naamini ule ushauri ni mzuri.

Naamini wapo wanawake wacha Mungu kweli ila wapo neutral kama hawa waroman catholic na walutheri na huwa hawajikuti sana na kujiona watakatifu kama walokole.

Mabinti wa kilokole mbona mpo hivyo? Au ni stresses za makanisani kwenu?

Aliyecopy Hotuba ya Obama na Kumpa Rais Buhari…Kufukuzwa Kazi

Wiki iliyopita Ikulu ya Nigeria kupitia kwa muandishi wa hotuba za Rais, iliingia kwenye skendo ya kunakili hotuba ya Rais Barack Obama na kumpa Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ambaye aliisoma kama ilivyo bila kujua, mpaka wapinzani walipoanzisha mzozo juu ya suala hilo.

Official responsible for Plagiarism of Obama's Speech to be sacked

Sehemu ya hotuba ya Rais Buhari iliyonakiliwa kutoka kwenye hotuba ya Rais Barack Obama aliyoitoa mwaka 2008 inasema “Change Begins With Me” Mabadiliko Huanza Na Mimi, ikifahamika kwa jina la Hotuba ya Ushindi.

Ikulu ya Nigeria imeomba radhi juu ya aibu iliyomkuta Rais wa nchi hiyo na kuahidi kumchukulia hatua kali za kinidhamu muandishi aliyesababisha.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Trust limesema kuwa kiongozi huyo msaidizi wa idara ya mawasiliano ya Rais, ataondolewa kazini kutokana na uzembe alioufanya. Muda mfupi tangu kutokea tatizo hilo, Taasisi ya Rais kupitia idara ya mawasiliano kwa Umma imeripoti kuwa itaweka software itakayokuwa ikigundua kama hotuba zote za Rais zimenakiliwa kutoka sehemu nyingine.

Msemaji wa Serikali ya Nigeria amesema >>>Tumepanga kuchukua hatua ya kuweka kifaa kitakachokuwa na uwezo wa kukagua na kugundua kama hotuba za Rais zimenakiliwa kutoka sehemu nyingine kabla ya kumkabidhi Rais,”

Kitendo cha Hotuba ya Rais Buhari kunakiliwa kutoka kwenye Hotuba za Rais Obama, kimewafanya vyama vya upinzani nchini humo kusema kuwa ipo siku Rais huyo atasaini nakala za kujiuzulu bila kujua kutokana na kutozikagua kabla ya kuzisoma.

Mwanamuziki Vanessa Mdee Ataja Ndoto yake Katika Muziki wa Bongo Flava

Mwanamuziki wa kike anayesumbua ndani na nje ya Bongo, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amesema ana ndoto kubwa.

Ndoto yake siku moja, kuwa msanii kutoka Tanzania atakayeshinda tuzo za heshima, Grammy.Anaamini kuwa, mwanzo wa kukaribia kuiishi ndoto hiyo umewadia.

Vee Money ni mmoja wa wasanii wa Afrika, waliochaguliwa kurekodi wimbo na mshindi wa Grammy na nyota wa RnB nchini Marekani, Trey Songz.

Shukrani kwa kipindi cha Coke Studio Africa (International Week) msimu wa 4, kinachomdondosha staa huyo.

Akiwa pia anawania tuzo ya Loeries za Afrika Kusini kwa kazi yake ya video bora, Niroge.

“Katika harakati zangu za kutafuta ushindi wa Grammy katika career yangu ya muziki, inanipa nguvu kufanya kazi kwa ukaribu na Trey Songz, ambaye alishawahi kushinda tuzo hiyo.” amesema Vanessa.
Msimu mpya wa Coke Studio utaanza mwezi ujao.